Nyisu Tech Solution inajumuisha timu thabiti ya wataalamu wa mifumo ya kompyuta, wasimamizi wa cloud servers na walimu wa programming. Tunajikita katika maeneo makuu matatu: kubuni na kutengeneza mifumo salama, kutoa huduma za hosting na usimamizi wa server, pamoja na kuendesha programu yetu ya **Programming Academy** ili kutoa mafunzo ya vitendo ya coding.

Tunaamini katika unyumbulifu na uwezo wa kubadilika kulingana na mabadiliko ya teknolojia na bajeti ya mteja. Kila suluhisho tunalounda au kulifundisha linalenga kuleta ufanisi mkubwa wa kiutendaji na kutengeneza fursa mpya za kiteknolojia.

Kupitia cloud server zetu thabiti, tunahakikisha tovuti zote tunazozijenga na kuzisimamia zinaendelea kuwa hewani 24/7 kwa kasi kubwa na ulinzi thabiti wa kiusalama.

HTML5 / CSS3
JavaScript (ES6+)
React / Next.js
Python / Django
PostgreSQL / MySQL
Academy Teaching
Server Management
Docker / Container

Dira Yetu (Vision)

Kuwa kituo kikuu cha kutoa huduma za kisasa za teknolojia na elimu ya vitendo ya mifumo nchini Tanzania na Afrika Mashariki, tukiwajenga vijana na biashara kukua kidijitali kwa njia salama na yenye ufanisi.

Dhamira Yetu (Mission)

Kutoa huduma bora na za kuaminika za kubuni mifumo (systems development), cloud hosting thabiti, na kutoa mafunzo yasiyo na kikomo ya coding ili kuwaandaa wataalamu thabiti watakaoleta mapinduzi ya viwanda vya kiteknolojia.

Maadili Yetu Ya Kazi (Core Values)

Ubunifu (Innovation)

Kila mfumo tunaotengeneza unazingatia ubunifu wa hali ya juu na kuangalia namna bora zaidi ya kurahisisha kazi kwa mtumiaji wa mwisho.

Uaminifu (Integrity)

Tunajenga mahusiano ya kudumu na wateja wetu kupitia uwazi, uaminifu wa gharama za hosting na mikataba ya kazi.

Ubora na Viwango

Hatufanyi kazi kwa kubahatisha. Kila code, template na server config inakaguliwa kuhakikisha inakidhi viwango vya kasi na usalama wa kimataifa.